Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii
wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa
ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo
kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.
Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba
mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda
tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya
Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa
muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni
wapi ametoka na wapi anakwenda.
Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks
iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati
ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani
Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya
Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.
Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla
haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention
zaidi kwenye soko la muziki barani Afrika.
Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii
wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla
ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii
Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi
ambazo zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia
kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini
hawazipati.
Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake
itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa
mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour
yake inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii
zimebaki siku tatu kufikia mwezi February.
Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni Afrika
Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na
haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye
kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya
collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.
Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa
kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya
iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi
husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii
kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla
hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?
Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo
amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi
South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata
wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour
kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.
Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna
ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki
linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram
msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost
kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine
wa Alikiba DM kua Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha
wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha
mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.
Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule.