Nay wa Mitego na producer aliyemtambulisha kwenye game, Mr T Touch
walikuwa na chemistry ya aina yake na walifanikiwa kutengeneza hits
nyingi.
Baada ya kufanya kazi kwa muda katika studio za Free Nation za Nay,
Touch aliamua kujiengua na kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe. Huko
bado anaendelea kufanya vizuri. Pamoja na kwamba hawafanyi tena kazi
pamoja, Nay anakiri kuwa Touch bado ni producer mzuri.
“Ni producer mzuri, nimefanya naye kazi kwa muda mrefu so sidhani
kama kutakuwa na kitu kipya cha ajabu toka kwake,” Nay alimuambia
mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove.
Hata hivyo Nay anadai tangu aondoke Free Nation bado hajasikiliza ngoma mpya za producer huyo.
SHARE THIS
0 maoni: