Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Sunday

 Mbwana Samatta aipatia Taifa Stars ushindi wa mabao 2-0

Mbwana Samatta aipatia Taifa Stars ushindi wa mabao 2-0

Mbwana Samatta amefanya kile ambacho watanzania wengi walikuwa wanatarajia akifanye, magoli mawili aliyofunga yameipa Stars ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kalenda ya FIFA iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Samatta alianza kuweka kambani dakika ya pili tu tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza baada ya kutoka na mpira nje ya box na kuwakusanya mabeki wa Botswana na kuingia nao kwenye box kisha kumtungua kwa mguu wa kushoto golikipa wa Botswana ambaye aliruka bila mafanikio.
Bao hilo lilidumu kwa dakika zote zilizobaki za kipindi cha kwanza huku mchezo ukiwa umechangamka kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili Botswana waliamua kuliandama goli la Stars kwa mashambulizi ya mara kwa mara kwenye goli la Stars na mara kadhaa walipoteza nafasi za kufunga.
Dakika ya 87 kipindi cha pili, Samatta alifunga goli la pili na la ushindi kwa Stars kwa mkwaju wa free-kick nje kidogo ya box la penati baada ya yeye mwenyewe (Samatta) kuangushwa nje kidogo ya eneo la penati box.
Licha ya kufunga magoli mawili, Samatta aliwa kwenye wakati mgumu kwa sababu mara nyingi alikuwa akichezewa rafu zilizosababisha wachezaji wa Botswana kuoneshwa kadi za njano. Samatta ilibidi atibiwe na daktari wa Stars baada ya kufanyiwa rafu wakati akijaribu kumtoka moja ya mabeki wa Botswana.
Umahiri wa golikipa wa Botswana Kabelo Dambe umeisaidia timu yake kupunguza idadi ya magoli kutokana na kuokoa michomo ya miwili ya Mbwana Samatta pamoja na Simon Msuva.
Taifa Stars itacheza tena mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi siku ya Jumanne March 28, 2017 kwenye uwanja wa taifa.
 Mbwana Samatta anamiliki mijengo sita Dar

Mbwana Samatta anamiliki mijengo sita Dar

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.
“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.

Monday

Uingereza huenda ikakosa fainali za kombe la dunia 2018

Uingereza huenda ikakosa fainali za kombe la dunia 2018

Chama cha soka duniani FIFA kinakataza Serikali kuingilia masuala ya soka na adhabu kali hutolewa kwa mwanachama yeyote anayekiuka jambo hilo. Bunge la Uingereza linataka kupiga kura ya kutokuwa na imani na chama cha soka cha nchini humo FA.

Hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo jambo hili linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia ,Endapo bunge litapiga kura wiki ijayo basi itaiweka Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la dunia la mwaka 2018.
Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na FA unakuja baada ya baadhi ya viongozi wa zamani wa FA kudai kwamba chama hicho kinashindwa kujiendesha.Katika barua ambayo viongozinwa zamani wa FA walimuandikia mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni bwana Damians Collin inaelezwa kwamba FA imekwama na imeshindwa kujiendesha.Inasubiriwa kwa hamu kuona nini kitatokea baada ya kikao cha bunge la Uingereza kutoa maamuzi yao kuhusu FA.
Kesi hii ya Uingereza haina utofauti na kesi iliyokuwa ikiwakabili Kuwait katika hatua ya kushiriki kombe la dunia 2018.Serikali ya Kuwait iliingilia masuala ya soka nchini humo.Wakiwa wamefika raundi ya tatu ya mechi za kufuzu kombe la dunia FIFA waliamua kuwatoa Kuwait katika mashindano hayo baada ya serikali yao kukiuka sheria za Fifa.
Uingereza ambao hadi sasa wako katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia kwani wanaongoza kundi lao la F. Uingereza wamebakiza mechi 6 tu kufuzu kombe la dunia lakini sheria za FIFA zinaweza kuwazuia kufuzu ama kuendelea na mechi zao kwa sasa.

Friday

Kilimanjaro Warriors kuingia kambini kujiandaa na Olimpiki 2020

Kilimanjaro Warriors kuingia kambini kujiandaa na Olimpiki 2020

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ inatarajiwa kuingia kambini Janauri 29, 2017 kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali za Olimpiki zitakazofanyika jijini Tokyo, Japan mwaka 2020.
Kambi hiyo ya wiki moja itafanyika kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.
Tanzania haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufanikisha mipango na taratibu.
Tanzania kwa sasa ina vijana wengi waliotokana na michuano ya Mradi wa kuibua na kukuza vipaji wa Airtel kadhalika na Cocacola ambao wamekuwa chachu ya maendeleo ya timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Vijana hawa wa Airtel, Copa Cocacola na Serengeti Boys wataungana na baadhi ya vijana waliofanya vizuri kwenye Ligi ya Vijana wenye umri wa chini miaka 20 kutoka timu za Ligi Kuu ambao wamezaliwa baada ya tarehe 1 Januari 1997 ili kuunda kikosi imara cha awali kuelekea kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo Japan, mwaka 2020.
Kwa kufuata utaratibu wa maandalizi ya Serengeti Boys na kwa kushirikiana na TOC timu hii itapewa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu ndani na nje ya nchi.

Thursday

FIFA kufanya mapinduzi ya soka, waweka wazi mpango wa kufuta offside na kubadili upigaji wa penati

FIFA kufanya mapinduzi ya soka, waweka wazi mpango wa kufuta offside na kubadili upigaji wa penati

Raisi mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kabisa.Infantino anaonekana kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake.Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 sasa Infantino amekuja na mpya.Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten amependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.
Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.
“sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha mashabiko na washambuliaji.
Kubadili upigaji wa penati.Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati.Kwa sasa adhabu ya penati mchezaji anauweka mpira mita kadhaa karibu na goli ma kuupiga.Lakini Van Basten anaona penati ibadilishwe.Anataka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.
Kupunguza adhabu mipira ya kushika.Van Basten anaona kama adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo.Na analiona kama tukio dogo lisilohitaji kadi nyekundu na anazani inapaswa ipunguzwe adhabu hiyo.Kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa.Adhabu kam ile ya tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati ukiingia golini Van Basten anataka kadi iwe ya njano.
Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi.Kama katika Rugby ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea na mwamuzi.
Style ya faulu ya mchezo wa kikapu.Katika mchezo wa kikapu pale mchezaji anapocheza faulu tano anatakiwa atoke uwanjani.Na sasa Van Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.
Kupunguza idadi ya mechi.Hii itafurahiwa sana na makocha wageni Uingereza.Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.
Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.
Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.
Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA, na sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliwa.
Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi

Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi

Bondia Francis Cheka ametangaza rasmi kuachana na mchezo wa ngumi na kujielekeza kwenye masuala binafsi ya kibiashara.
Mwanandondi huyo kutoka Morogoro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa ITV mjini Morogoro kuhusu taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii vikimhusiha na utapeli wa kukimbia ulingoni Dec 25 mwaka huu huko jijini Dar es Salaam, alikotakiwa kupigana na bondia Dula Mbabe,ambapo amebainisha kutofika ulingoni siku hiyo hakukumaanisha kuhofia pambano hilo bali ni kutokana na promota wake Kaike Selagi kutomlipa fedha zake zote kama walivyokubaliana, ambapo amedai alipaswa kulipwa milioni tisa, lakini hadi wanamaliza kupima uzito alikua amepewa milioni tatu pekee.
Akizungumzia azma ya kuachana na ngumi,Cheka amesema kwa muda mrefu amekuwa akipigana bila mafanikio kutokana na kudhulumiwa na waandaaji au kulipwa tofauti na makubaliano sambamba na misukosuko ya hapa na pale anayofanyiwa na wapinzani wake na kwamba anaamini wapo baadhi ya watu waliolenga kumshusha kwenye ngumi badala ya kumtengeneza bondia mwingine mwenye uwezo na kumpiga na kwamba kwa sasa atajielekeza kufanya biashara zake na kuahidi ushirikiano kwenye mchezo wa ngumi ili kukuza na kuendeleza mchezo huo.

Saturday

Sam Allardyce ateuliwa kuwa kocha mpya wa Crystal Palace

Sam Allardyce ateuliwa kuwa kocha mpya wa Crystal Palace

Klabu ya Crystal Palace ambayo inashriki ligi kuu ya Uingereza, hatimaye imemtangaza Sam Allardyce kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kumfuta kazi kocha Alan Pardew wakati ambapo klabu hiyo iko katika nafasi ya 17 katika ligi hiyo.
Sam Allardyce amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu, Big Sam ambaye aliingia matatani na chama cha soka nchini Uingereza (FA) na kutumuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, baada ya kuwaeleza waandishi wa habari wa gazeti la Daily Telegraph waliojifanya wafanyabiashara kuwa ni rahisi kuizunguka sheria ya chama cha soka nchini Uingereza (FA).
Rais wa FIFA kuja na mikakati mipya kwenye klabu bingwa kuanzia 2019

Rais wa FIFA kuja na mikakati mipya kwenye klabu bingwa kuanzia 2019


Rais wa shirikisho la soka ulimwengu FIFA Gianni Infantino amesema anapanga kuboresha michuano ya klabu Bingwa dunia kutoka timu 7 hadi timu 32 lengo likiwa ni kuboresha michuano hiyo ili ilete mvuto tofauti na ilivyokuwa sasa na huo mpango wake anataka uanze mwaka 2019.
Infantino aliliambia gazeti la michezo la Gazzetta dello Sport na lile la El Mundo Deportivo kwamba anaamini hilo linawezekana.
Michuano ya Kombe la Dunia la klabu mwaka 2015 iliyofanyika nchini Japan kama ilivyo ada, iliingiza faida kupitia matangazo kiasi cha dola million 20 ambacho kilionekana ni kiasi kidogo kwa kuwa michuano ya mwaka 2014 iliyofanyika nchini Morocco iliingiza hadi dola million 40.
Rais huyo anaamini kubadili mfumo huo kutafanya kuongeza mvuto wa mashindano hayo.

Sunday

TAIFA STARS KUPIGWA 3-0 NA ZIMBABWE

TAIFA STARS KUPIGWA 3-0 NA ZIMBABWE


Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mechi yake na Zimbabwe kwa kufungwa 3-0 katika mchezo wa kirafiki.
Zimbabwe ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Knowledge Musona dakika ya tisa kabla ya mshambuliaji Matthew Rusike kuongeza bao la pili.
Goli la mwisho la Zimbabwe liliwekwa kambani na Nyasha Mushekwi katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili.
Newz: Mambo Matano Yaliyo Iangusha Timu Ya Simba Yasome Hapa

Newz: Mambo Matano Yaliyo Iangusha Timu Ya Simba Yasome Hapa

  
  1. Eneo la kiungo la Simba

Safu ya kiungo ya Simba ilibadili mchezo wao wa pasi nyingi hasa baada ya Yanga kuanza mchezo kwa kasi wakitumia mipira mirefu kutoka kwa Kamusoko kwenda kwa Niyonzima na Ngoma kitu ambacho kilimfanya Tambwe awe huru zaidi na madhara ya Ngoma yalionekana kutokana na usumbufu wake akamsababishia kadi Nyekundu mlinzi Banda.

 

  1. Morali ya wachezaji baada ya Kadi  Nyekundu

Wachezaji wa simba walionekana  kutokukubaliana na kadi ya Banda hali ambayo iliwatoa mchezoni kwa muda akiwemo kiungo Mwinyi Kazimoto ambaye hakucheza kama alivyozoeleka kwenye Mechi za hivi karbuni na hali hii ilikuja baada ya kiungo Majavi kulazimika kurudi nyuma kucheza beki na Juuko..Kiungo cha Simba kilikatika na kutoa nafasi kwa Niyonzima kucheza pamoja na Kamusoko wakiwalisha vizuri washambuliaji wao.

 

  1. Kasi na Utulivu wa Donald Ngoma

Ngoma amechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa jana baada ya kuwa msumbufu na muda wote akikaa eneo la kumi na Nane ya Simba kitu ambacho kiliwanyima uhuru mabeki wa simba kuanziana pasi fupi na matokeo yake aliweza kukaa eneo zuri na akatumia makosa ya Kessy na kuandika bao la kwanza.

 

  1. Mabadiliko ya Kocha Mayanja 

Baada ya mapumziko Kocha wa simba aliamua kupumzisha Kazimoto ambaye alionekana kuumia na kucheza chini ya kiwango lakini hakupiga vizuri hesabu zake..kwangu mimi naona alitakiwa kuingiza beki atakaye cheza na Juuko kisha kumpandisha Majavi kwenye nafasi ya kiungo wa kati ili kusaidiana na Mkude lakini haikuwa ivyo aliona amwingize kiungo ambaye bado hakuwa na uzoefu wa pambano kubwa kama hilo na matokeo yake alipwaya na kumulazimu Ajib kurudi kusaidia viungo huku mbele wakimwacha Kiiza peke yake.

 

  1. Kuingia kwa Mwashuya na Simon Msuva 

Bao hili liliwatoa simba mchezoni na kuwafanya wacheze nyuma zaidi bila ya kuwa na mashambulizi ya uhakika.

Mechi ilikuwa nzuri kila upande umejaribu kuonesha nini ambacho wamevuna kwa walimu wao na hatimaye bahati ikaanguka kwa Yanga na kuibuka na pointi zote sita msimu huu.

CHANZO_mtembezi.com