Msanii wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi ambaye alikuwa mbunifu wa mavazi
ya Diamond Platnumz amesema si kweli alikuwa anapinga ujio wa mtandao wa
wasafi.com kitu kilichopelekea kutimuliwa WCB.
Q Boy ameiambia kipindi cha cha The Play List cha Times FM, wakati mtandao huo unaanzishwa yeye tayari alikuwa nje ya WCB.
“Suala la wasafi.com hata walipozindua mimi sikuwepo. Hata maandalizi
for real nilikuwa mbali na vikao ambavyo walikuwa wanafanya kwa sababu
nilikuwa out of wasafi na nilikuwa nimeshanza kufuatilia ishu zangu
lakini nilikuwa na fununu kuwa wasafi wanafungua mtandao,” amesema Q
Boy.
Katika hatua nyingine Q Boy amesema sababu ya wimbo wake mpya
‘Karorero’ kutokuwepo katika mtandao huo ni kwamba tayari alikuwa
ameshauuza kwa watu wengine.
“Wimbo wangu wa pili sikuupeleka ila bosi Tale aliniandikia kwenye
Whats App fanya ulete wimbo wako kwenye wasafi .com lakini mimi nilikuwa
nimeshakaa chini na watu ambao nilitaka kuwapa caller tunes, so
sikuweza kuchanganya,” ameongeza.
0 maoni: