-
Eneo la kiungo la Simba
Safu ya kiungo ya Simba ilibadili mchezo wao wa pasi nyingi hasa baada ya Yanga kuanza mchezo kwa kasi wakitumia mipira mirefu kutoka kwa Kamusoko kwenda kwa Niyonzima na Ngoma kitu ambacho kilimfanya Tambwe awe huru zaidi na madhara ya Ngoma yalionekana kutokana na usumbufu wake akamsababishia kadi Nyekundu mlinzi Banda.
-
Morali ya wachezaji baada ya Kadi Nyekundu
Wachezaji wa simba walionekana kutokukubaliana na kadi ya Banda hali ambayo iliwatoa mchezoni kwa muda akiwemo kiungo Mwinyi Kazimoto ambaye hakucheza kama alivyozoeleka kwenye Mechi za hivi karbuni na hali hii ilikuja baada ya kiungo Majavi kulazimika kurudi nyuma kucheza beki na Juuko..Kiungo cha Simba kilikatika na kutoa nafasi kwa Niyonzima kucheza pamoja na Kamusoko wakiwalisha vizuri washambuliaji wao.
-
Kasi na Utulivu wa Donald Ngoma
Ngoma amechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa jana baada ya kuwa msumbufu na muda wote akikaa eneo la kumi na Nane ya Simba kitu ambacho kiliwanyima uhuru mabeki wa simba kuanziana pasi fupi na matokeo yake aliweza kukaa eneo zuri na akatumia makosa ya Kessy na kuandika bao la kwanza.
-
Mabadiliko ya Kocha Mayanja
Baada ya mapumziko Kocha wa simba aliamua kupumzisha Kazimoto ambaye alionekana kuumia na kucheza chini ya kiwango lakini hakupiga vizuri hesabu zake..kwangu mimi naona alitakiwa kuingiza beki atakaye cheza na Juuko kisha kumpandisha Majavi kwenye nafasi ya kiungo wa kati ili kusaidiana na Mkude lakini haikuwa ivyo aliona amwingize kiungo ambaye bado hakuwa na uzoefu wa pambano kubwa kama hilo na matokeo yake alipwaya na kumulazimu Ajib kurudi kusaidia viungo huku mbele wakimwacha Kiiza peke yake.
-
Kuingia kwa Mwashuya na Simon Msuva