“Hata mimi wakati sina kitu yaani, unakuta unampigia simu [Chidi Benz] ‘ebana eh inakuaje uko wapi? Hebu njoo tukutane Ubungo.’ Unaenda unachezea labda shilingi 50 fulani, shilingi 30,” alisema Izzo kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM.
Izzo anadai kuwa pamoja na misaada ya kifedha ya hapa na pale, Chidi alikuwa mtu aliyekuwa akimpa ushauri mwingi uliomjenga kimuziki.
“Chidi atabaki kuwa big brother, kuna mambo ya duniani kila mtu ana mitihani yake lakini hata mimi namuombea, nammiss, game imepoa Chidi ni bonge ya rapper, hamna ambaye hajui, kuna vijana wengi sana ametusaidia,” amesisitiza Izzo.
0 maoni: