Diamond Platnumz amesema kwa sasa redio na TV si vyombo
anavyovitegemea sana kwaajili ya promotion pindi anapokuwa akiachia
nyimbo.
“Mimi nikiwa natoa nyimbo yangu, promotion yangu siwazi redio wala
siwazi TV, ever. Promotion yangu ya kwanza mimi nawaza nyimbo iwafikiaje
watu, kuna mitandao ya kijamii, kuna digital platform nyingi,” staa
huyo alisema kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz.
Alidai kuwa zama za kundi Fulani la watu likiamua kumrudisha nyuma msanii, halipo tena kwa wasanii wenye nguvu kama yeye.
“Tufute zile ‘naweza nikamdhuru mtu fulani ninavyotaka mimi’ vile vitu havipo tena,” aliongeza.
SHARE THIS
0 maoni: