Thursday

Mpenzi mpya wa Shilole: Mimi kuchora tattoo ya Shilole ni moyo wangu tu umetaka kufanya hivi

Mpenzi mpya wa Shilole ambaye ni mfanyabiashara wa nguo, Adam, amefunguka na kuzungumzia jinsi wanavyopendana na Shilole.
Kijana huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hamwangalii Shilole alipotoka bali anaangalia hapo alipo kwa sasa na anamuomba sana Mungu ili waweze kufika mbali zaidi.
“Mimi sijafuata boost kwa Shilole bali nimefuata mapenzi na mimi naweza kusema kuwa hayo ya nyuma siyaangalii bali naangalia hapa tulipo,” alisema Adam
Aliongeza “Kwa sasa na mimi kuchora tattoo ni moyo wangu tu umetaka mimi kufanya hivi, na ninachomuomba Mungu ni kufika mbali tu na yeye basi,”
Hapo awali Shilole kabla ya kuingia kwenye mahusiano na kijana huyo alikuwa anatoka na msanii chipukizi wa muziki aitwae Hamadai.

SHARE THIS

0 maoni: