Monday

Mama Wema Sepetu ashinda Polisi kujua hatima ya mwanaye

Sakata la baadhi ya wasanii wakubwa nchini kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya limezidi kuchukua sura mpya, huku mzazi wa Wema Sepetu akishinda polisi kujua hatima mwanaye.
Akiongea huku akiwa kama mtu aliyepatwa na hamaki mama mzazi wa Wema Sepetu, alisema kwa sasa anasubiri kauli ya Polisi ili aweze kujua kama mtoto wake atafikishwa mahakamani au laa.
Alisema kitendo cha kukamatwa mtoto wake na kuwekwa ndani kimemuumiza kama mzazi ingawa kwa sasa hana la kufanya zaidi ya kusubiri uamuzi wa vyombo vya dola.
“Kama mzazi nimeumia sana ila kwa sasa ninawaomba mniache maana siwezi kuongea kitu chochote kuhusu hili, hadi hapo polisi itakapotoa maamuzi yao ya uchunguzi wanaoufanya, ndiyo nitajua nini niseme,” mama Wema aliliambia gazeti la Mtanzania.
Baada ya kutoa kauli hiyo mama huyo alionekana ni mtu mwenye msongo ambapo muda wote alikuwa amekaa kimya tofauti na ilivyo kawaida yake ambapo huwa ni mtu mwenye uchu.

SHARE THIS

0 maoni: