Saturday

Rais Magufuli amkubalia DC aliyeomba kujiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjibu Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora aliyeomba kujiuzulu wadhifa huo.
Katika majibu yake Rais Magufuli ameridhia uamuzi huo na kwamba uteuzi wa mtu mwingine atakayejaza nafasi hiyo utafanyika baadaye.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa imesema
“Ombi la Bw. Gabriel Simon Mnyele aliyeomba kujiuzulu wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora limekubaliwana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora itajazwa baadaye.”
Taarifa za kujiuzulu kwa mkuu huyo wa wilaya zilianza kusambaa jana zikidai kuwa aliaga katika Kamati ya Madiwani wa CCM na kamati ya siasa ya wilaya, pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kuwa ameamua kuchia ngazi, bila kueleza sababu za uamuzi huo.
Hata hivyo baadaye kulitokea utata baada ya kusambaa kwa taarifa za yeye kukanusha kufanya uamuzi huo, lakini sasa ni dhahiri kuwa Bw. Gabriel Simon Mnyele siyo mkuu wa wilaya hiyo tena.

SHARE THIS

0 maoni: