Baada ya uteuzi wa Rais Magufuli jana wa Mwenyekiti wa chama cha ACT
Wazalendo, Anna Mghwira kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kulikuwa na
mijadala mizito mitandaoni na hata kwenye vyombo vya habari juu ya
uteuzi huo huku wengi wakimtaka Mbunge pekee wa chama hicho, Zitto Kabwe
atolee ufafanuzi juu uteuzi huo hatimae leo ametoa kauli yake ya kwanza
kuhusu uteuzi huo.
Zitto Kabwe amesema amezipokea taarifa hizo kutoka mitandaoni na
kwenye vyombo vya habari lakini bado Chama cha ACT wazalendo hakijafanya
mawasiliano na Mghwira anmbaye yupo nje ya nchi mpaka atakaporejea
ndipo chama kitatoa msimamo wake juu ya uteuzi huo.
“Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama
chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu
tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti
yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana
nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.“ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hata hivyo Zitto Kabwe amewataka Wanachama wa chama cha ACT wazalendo
luwa watulivu kwa kipindi hiki mpaka hapo taarifa rasmi itakapotolewa
pindi atakaporejea nchini.
“Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na
Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.“ameandika Zitto Kabwe.
0 maoni: