TID: UHALISI WA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEPOTEA
Msanii mkongwe wa muziki wa bongofleva TID amedai uhalisia wa muziki huyo umepotea baaada ya baadhi ya wasanii kuiga muziki wa nje.
Akiongea katika kipindi cha Ubaoni cha EFM Alhamisi hii, TID amesema muziki wa bongofleva umetokana na mchanganyiko wa muziki wa hip hop na RnB.
“Uhalisia ya muziki wa bongofleva umepotea watu sasa hivi wanataka kuimba kama Wanigeria, watu wanataka kuiga vitu vya nje lakini wakumbuke kwamba bongofleva maana yake ni mchanganyiko wa muziki wa hip hop na RnB,” alisema TID.
Muimbaji huyo amesema aliamua kuandika wimbo ‘confidence’ ili kuwaonyesha vijana wanatakiwa kufanya nini kwenye nyimbo zao.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amesema anashangaa kuona waandaaji wa tuzo za muziki nchini kushindwa kutoa tuzo kwa msanii wenye mchango mkubwa kwenye muziki.
“Ni mara chache sana kwenye tuzo zetu kushuhudia tuzo za heshima zinatoka kwa ‘legends’ wa muziki wetu kutambua mchango wao, hata aliyeanzisha tuzo za muziki za Kilimanjaro marehemu James Dandu sijashuhudia akipewa heshima yake tuzo hizi zinapofanyika.” alisema TID.
0 maoni: