Friday

MREMA AMFIKISHA MKUU WA GEREZA LA DODOMA KWA WAZIRI MKUU


Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amemuandikia barua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kulalamikia jeshi la magereza mkoa Dodoma kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema kuwa amesikitishwa sana na kitendo hicho kinachodaiwa kuwa ni agizo kutoka uongozi mkuu wa Magereza.
“Leo kuna watu ambao wapo magerezani wamelipiwa tayari, mimi nimeona nisinyamaze, napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalo tatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?.
“Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema.
Hata hivyo Mrema alisema mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya Parole katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo.

SHARE THIS

0 maoni: