Thursday

WatsUp Awards: Diamond, Alikiba, Navy Kenzo na Harmonize washinda

Majina ya washindi wa Watsup TV Music Video Awards (WAMVA) yametangazwa mjini Accra Jumatano hii. Jumla ya washindi 22 walipatikana kati ya washiriki 170 waliokuwa wametajwa.
Diamond ameibuka na tuzo kubwa zaidi ya ya African Video of the Year na wimbo wake Kidogo aliowashirikisha P’Square. Yeye ndiye aliyeibuka na ushindi mwingi zikiwemo Best African Combo Video ma Best African Male Video.
Alikiba ameibuka na tuzo mbili, BEST EAST AFRICAN VIDEO na BEST AFRICAN RnB VIDEO kupitia video ya wimbo Aje. Navy Kenzo wamechukua BEST AFRICAN GROUP VIDEO na Harmonize, BEST AFRICAN NEW COMER VIDEO.

SHARE THIS

0 maoni: