Friday

Wakuu wa mikoa 7 kutumbuliwa iwapo watashindwa kumaliza tatizo la madawati


Serikali imetoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa mikoa yote nchini ambayo haijamaliza tatizo la madawati kwa wanafunzi wa shule za serikali za msingi na sekondari zilizopo katika mikoa hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na Bank ya NMB ambayo yatasambazwa nchi nzima.
Aidha Simbachawene amesisitiza kwamba mikoa itakayoshindwa kumaliza zoezi hilo ndani ya muda waliopewa hicho kitakuwa kielezo tosha kwa viongozi hao kuwa wameshindwa kwenda na kasi ya uongozi wa awamu ya tano.
“Kwa mikoa hii ambayo nimeitaja haijafanya vizuri nawapa deadline mpaka Januari wawe wamemaliza vinginevyo watakuwa wameprove kwamba hawaiwezi kasi ya serikali ya awamu ya tano,”alisema Simbachawene.
Mikoa ambayo haijafanya vizuri kwa upande wa madawati ni pamoja na Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Dodoma, Rukwa na Simiu huku akisema kuwa ile ambayo haijatajwa ina tatizo dogo ambalo wanauwezo wa kumalizia.

SHARE THIS

0 maoni: