Mwanamke ambaye amemfanya rapa Nay wa Mitego aandike wimbo ‘Sijiwezi’
hataki habari za kuuzishwa sura katika mitandao ya kijamii kama wapenzi
wengine wa rapa huyo waliopita.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay amedai hawezi kufanya kitu
ambacho hapendi mwanamke huyo na ataendelea kuheshimu maamuzi yake huku
akikiri kuwa ni jambo gumu kwake kwa kuwa alishazoea kushare picha za
wapenzi wake katika mitandao ya kijamii.
“Huyu niliye naye kwa sasa hataki kusikia kuhusu masuala ya kuweka
sijui picha kwenye mtandao,” alisena Nay. Ni mwanamke fulani ambaye ana
msimamo wake kuhusu maisha yake, hataki masuala ya kuyumbishana
yumbishana kwenye mapenzi,”
Rapa huyo amedai bado wanaendelea kuchunguzana lakini anadhani
huwenda akawa ni mwanamke wa kwanza mwenye tabia za tofauti kuwa naye na
huenda akafika naye mbali zaidi.
0 maoni: