Najua huwa tunatumia muda mwingi sana
vijiweni tukiongelea, sehemu gani nzuri ya kukutana na wanawake, jinsi
ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini cha kuongea na kufanya ili
akuelewe na mrembo awe wako, Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea
huwa ni kama theluji kwenye mlima Kilimanjaro, ila volkano yenyewe huwa
ni jinsi ya kuwafanya wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na
hizi hapa ni njia tano za kuwa wapekee na kuwafanya watoto wenyewe wa
kike wawe wanakuhangaikia.
Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia
hizi hakikisha hauzichukulii juu juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye
akili yako, maana unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote
tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu wanawake.
Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.
Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni
kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na mwanaume wa kweli, onyesha
kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa Kutongoza toka moyoni bila hata
kufikiria utaongea nini au kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata
kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa
mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza
kujitambulisha, “Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba”, mwenyewe anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.
Namba 2. Muonyeshe changamoto.
Mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa
umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji
kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye
kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo),
mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye
mapenzi yanamuendesha.
Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.
Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni
mwanaume wa aina flani, kuna uhakika mkubwa ataendelea kukufikiria kuwa
wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo
we ni mwanaume yule anaye lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala
tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi,
na unajua wanawake wanahisia gani na wanaume wa aina hii. Kwahiyo
ukianza na maswali ya kuonyesha tabia ya kifala, patishia huyo mwanamke
ataanza kukufikiria kuwa utakuwa na tabia hizo hizo kwa kipindi chote
cha maisha yako, na huo ndo utakuwa mwisho wako.
Namba 4. Usimfuatilie sana.
Usipoonana na mtu sana mara kwa mara
hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke
utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako, iwapo ungeitumia hata kwa
naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo ukiwa
unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubiri na kumpa muda
mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia, utafanya siku zote
uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja.
Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani. Wanawake
wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa
anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake
huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi
cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha
wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali
ambayo hazihitajiki
0 maoni: