Rapper wa Perfect Combo, Joh Makini amedai kuwa vyombo vya habari
wakishirikiana na wasanii wa muziki inabidi wabadilishe mfumo uliopo kwa
sasa kwenye muziki.
Joh ameiambia Bongo5 kuwa kwenye tuzo mbalimbali kubwa duniani pamoja
na chati za muziki unaweza ukaona msanii mmoja anaingiza nyimbo zaidi
ya moja kitu ambacho hapa nchini kimekuwa kigumu kufanyika.
“Nafikiria sisi tukishirikiana na media tukubaliane na huu wakati
kwamba sio wakati wa watu kushangaa kwanini msanii mmoja ana nyimbo tatu
wenye Top 10 au kwanini msanii mmoja anakuwa kwenye category moja mara
tatu. Unajua wenzetu kwenye grammy au nchi zilizoendelea hawashangai
hili. Nenda Billboard unaweza ukakuta msanii ana nyimbo tano kwenye Top
10, lakini hapa bongo wanasema nyimbo yake namba moja halafu uingize
nyingine? ” amesema Joh.
“Hapana huwezi kuweka nyimbo mbili za msanii mmoja kwenye nafasi ya
kwanza, ya pili na ya tatu, ni lazima hayo mambo yaishe. Kama kuna mtu
anastahili kuwa na nyimbo tano kwenye chati na ni kali inabidi ziwepo
kwa sababu hiyo inawafanya watu wengine waingie studio kufanya kazi
nzuri zaidi,” ameongeza.
0 maoni: