Sunday

Mastaa wapamba uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ‘Give IT TO ME’

Mastaa wa muziki, filamu pamoja na viongozi wa serikali Jumamosi hii walipamba usiku wa uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ‘Give IT TO ME’.
Belle 9 akizungumza na waandishi wa habari
Tafrija hiyo fupi ambayo iliandaliwa na kampuni ya muimbaji huyo,Vitamin Music Group Limited, iliwakutanisha wadau mbalimbali wa muziki pamoja na waandishi wa habari.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ni mmoja kati ya viongozi wajuu waliohudhuria uzinduzi huo.
Akiongea katika uzinduzi huo, Belle aliishukuru team nzima ya Vitamin Music Group Limited kwa kufanikisha tukio hilo pamoja na wadau mbalimbali ambao walijitokeza usiku huyo kwa ajili ya kumsupport. Angalia picha.
Navy Kenzo wakiwa ndani ya nyumba
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Diwani wa kata ya Mwanga Kigoma, Baba Levo

Millard Ayo akishow love na mdau

Joh Makini akiwa na Mx Carter
Mbunge Ridhiwani Kikwete (kwanza kulia) akiwa na mmoja kati ya wafanyakazi wa Vitamin Music Group Limited (katikati) pamoja na Joh Sambila (kwanza kushoto)




SHARE THIS

0 maoni: