Friday

‘Too Much’ ya Darassa yajiwekea rekodi yake

Kufanya vizuri kwa wimbo mpya wa Darassa ‘Muziki’ umezidi kuzipa nguvu nyimbo zingine za rapper huyo.
 
Na sasa, video ya wimbo wake wa ‘Too Much’ aliyoiachia mwezi Julai mwaka huu, imefanikiwa kufikisha views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube.
Hii ni video ya pili kwa Darassa kutazamwa mara nyingi zaidi baada ya ‘Muziki’ ambayo mpaka sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 1.7 kwenye mtandao huo. Nao wimbo mwingine, Kama Utanipenda aliomshirikisha Rich Mavoko, unakaribia kufikisha views milioni moja.

SHARE THIS

0 maoni: