Wednesday

Man Water atoa sababu zilizowafanya washindwe kumrudisha 20%

Mtayarishaji wa muziki nchini Man Water amefunguka sababu iliyowafanya washindwe kukamilisha mipango yao ya kumrudisha msanii wao 20% kwa mwaka huu.
Water amekiambia kipindi cha E-News cha EATV kuwa matatizo ya kufiwa ndio yalisababisha washindwe kukamilisha mipango yao kwenye muziki.
“Kwanza kabisa mipango ambayo tulikuwa tumepanga ilishindwa kutimia. Tulikuwa na mipango ya kufanya video na tunaangalia video ingekuaje, bajeti ipoje yaani kulikuwa na mambo mengi sana wakati huo huo 20% alifiwa na dada yake, mimi mwenyewe nikafiwa, yaani kulikuwa na mambo mengi sana hivyo kuahirisha kukawa kwingi sana. Unakuta upande mmoja kukiwa sawa kwingine kuna kuwa siyo, hivyo muda huu tunaomba Mungu mengine yasitokee yale ya dharura ili katika hii new page tujue tunafanya nini,” amesema Water.
Mtayarishaji huyo ameongeza kuwa mpaka sasa 20% ana nyimbo tano ambazo zipo tayari kwenye store yake. Mpaka sasa msanii huyo ameachia wimbo mmoja pekee tangu aliposaini mkataba na lebo yake hiyo ya zamani ‘Combination Sound’ mwezi Julai mwaka huu.

SHARE THIS

0 maoni: