Thursday

Gabo Zigamba: Mungu mwenyewe atakuja kuinusuru tasnia ya filamu sio sisi

 gabo
 Msanii wa filamu Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amedai hakuna msanii wa filamu ambaye ataweza kuinusuru tasnia ya filamu kutokana na wasanii wa filamu kukosa umoja.
Alisema hayo wiki hii wakati alipowatembelea wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani) na kuzungumza nao mambo mbalimbali pamoja na kuwaeleza changamozo zinazoikabili tasnia ya filamu.
“Wasanii tuna umoja wa kuusema lakini mioyo yetu haina ukweli, kila mmoja anataka kufanya kitu peke yake. Kwahiyo kuna changamoto nyingi soko halipo rasmi, unaweza ukawa unaandaa filamu na usijue unamuuzia nani?. Ukijua unamuuzia nani haujui atakupa kiasi gani?, ukijua una muuzia nani haujui atakulipa katika mtiririko upi. Unafanya wewe filamu bei anapanga yeye soko haliwezi kwenda sawa,” alisema Gabo.
Aliongeza, “Sisi tuna umoja wa Nyumbu tupo 20 lakini Simba mmoja anatutoa jasho. Kwahiyo hatuna sehemu ya kusema wala hakuna mtu wakutusemea, nani atasema?. Kwahiyo ule umoja wetu ungekuwa na kauli moja tungefanikiwa, kiongozi akiniita mimi naenda kusema shida zangu, akimuita Kajala tena ataenda kusema shida zake. Lakini huwenda mimi na Kajala tungesema shida moja labda tungesaidiwa, kwahiyo kwa namna hii Mungu mwenyewe atakuja kuinusuru tasnia ya filamu lakini sio sisi,”
Pia muigizaji huyo alisema anajipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Siyabonga’.

ULIITAZAMA HII?;  Diamond na Zari kukava jarida la Mamas and Papas la SA


SHARE THIS

0 maoni: