Bella anaamini kuwa ushawishi wa wasanii hao wawili haupingiki na kuwachukia ni kujipa matatizo bure.
“Kwanini Diamond anapendwa? Diamond hapendwi si sababu ya kubeba vyuma tu, unaweza ukabeba vyuma na usipendwe vilevile. Angalia muziki wa Diamond kwanini unapendwa. Diamond anapendwa si kwaajili ya skendo kwasababu zile skendo pia huwa zinamuumizaga. Jamaa anatengeneza muziki mzuri, kubali ukatae,” alisema Bella kwenye mahojiano na Lake FM ya Mwanza.
“Mimi napenda anayefanya vizuri. Mimi kila nikitaka kutoa ngoma lazima napima ngoma ya Diamond, nitaangalia anaimba nini, kwanini watu wanampenda? Naangalia Alikiba, kwanini watu wanampenda, kaimba nini, naanza kupima ngoma zao. Halafu mimi natafuta, sio niimbe kama Diamond, sio nifanye kama Alikiba, natafuta njia pale katikati. Ukitaka baraka wakubali kwanza wanaokubalika,” alisisitiza.
UMEITAZAMA HIYO HAPOCHINI?:WIMBO WA DARASSA ULIVOSABABISHA AJARI NJIANI
0 maoni: