Diamond Platnumz ni mfanyabiashara kwenye muziki asiyeogopa ‘kutake
risk’ kwaajili ya kukamilisha azma yake, hata kama uamuzi atakaouchukua
unaweza ukaleta mzozo ndani ya familia yake.
Katika kunogesha tamasha lake kubwa la Wasafi Beach Party, hitmaker
huyo anamdondosha hasimu mkubwa wa mchumba wake Zari, Huddah Monroe.
Kama umesahau, Huddah aliwahi kuingia kwenye bifu kali na Zari baada ya
kudai kuwa amewahi kutembea na Diamond na kwamba staa huyo ni ‘mali ya
umma.’
Diamond ameweka picha ya mrembo huyo kwenye Instagram akiwa ameipa kamera mgongo na kuwataka mashabiki wake kubashiri ni nani.
Hii ni picha nyingine ya Huddah akiwa na vazi hilo:
Katika kuthibitisha kuwa anakuja, mrembo huyo alipost video Instagram
akiiimba wimbo maarufu wa Darassa, Muziki na kuandika: Coming HOME
soon…
Niliota naolewa TZEEE,Single men mkuje kwa wingi tukamilishe ndoto
Na blah blah blahhh Sitaki kusikia…. Kamwili kangu kanatosha kujigamba.. #mistressofalltrades.”
Tukurudishe nyuma kwenye bifu ya Zari na Huddah kwa ujumbe huu ambao mrembo huyo wa Kenya aliupost Snapchat July 21, 2016.
SHARE THIS
0 maoni: