Huenda mtoto wa Young Dee, Tammy akawa amewarudisha tena karibu Young
Dee na Amber Lulu. Wawili hawa waliwahi kuwa wapenzi lakini kwa mujibu
wa mwanamitindo huyo alipoongea na U-Heard ya Clouds FM alionyesha kuwa
tayari wameachana na rapper huyo.
Lakini kutokana na ujumbe aliouandika model huyo kwenye picha
aliyoiweka kwenye mtandao wa instagram unaonyesha kuwa sasa kila kitu
kipo sawa kati yao na ameahidi kumlea mtoto wa Dee kwa mapenzi yote.
“Tammy wetu Nakulea mwenywe mom nakupromise ntakuwa mom mdogo bora kabsaa watashangaa,” ameandika Amber kwenye mtandao huo.
Hata hivyo kwa sasa Young Dee anadaiwa kuwa na mahusiano na mpenzi wake wa zamani Tunda.
SHARE THIS
0 maoni: