Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.
Katika
utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda
kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara tano zaidi
ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine walizaa
watoto wafu.
Utafiti
huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000
wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.Hata hivyo, utafiti
mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa
mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto wafu wanaozaliwa katika
nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.
Mkuu
wa utafiti huu,Louise O'Brien kutoka chuo kikuu cha Michigan, nchini
Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito hupunguza
uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina mama
wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na
gharama yoyote ile.
Tabia
hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri
kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.
Matokeo
ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto
wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu
kwa wanawake wajawazito.
Siku
zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa
upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito
mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto
huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.
Utafiti
huu uliofanyika nchini Ghana unaunga mkono utafiti uliofanyika hivi
karibuni nchini Australia unaojulikana kama Sydney Stillbirth Study
ambao ulisema ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito wako
kwenye hatari ya mara sita zaidi ya kuzaa watoto wafu.Utafiti huu wa
Australia ulifanyika kwa miaka mitano na ulihusisha wanawake wajawazito
295 kutoka katika hospitali nane nchini Australia.
Naye
mtafiti mkuu katika utafiti huu Dr. Adrienne Gordon, kutoka Sydney's
Royal Prince Alfred Hospital amesema “Tafiti za awali zilionyesha ya
kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito, hupunguza mzunguko
wa damu unaotakiwa kwenda kwa mtoto.Lakini pia ni vizuri kwa wanawake
ambao ni wajawazito kutotaharuki kama wakati mwingine watalala
chali.’’Kutokana na idadi ndogo ya wanawake wajawazito waliohusishwa
kwenye utafiti huu sisi wana Tanzmed tunachelea kusema ya kwamba ni
vigumu kusema utafiti huu umetoa mapendekezo sahihi ya namna ya kulala
kwa wanawake wajawazito.
Pia
kutokana na kutoangalia muda ambao wanawake hao walilala wakiwa chali
(mfano kama walilala masaa 4,6 au 8 kwa siku na kwa siku ngapi) na
tofauti ya hatari kati ya wanawake wajawazito waliolala muda mfupi na
mrefu, hivyo tunawaambia wanawake wajawazito kutohofu kama watalala
chali lakini ni bora kuchukua tahadhari mapema.Tafiti hii inatoa
changamoto kwa watafiti wetu wa afya kuangalia jinsi ya kufanya tafiti
kama hizi katika mazingira ya kwetu.
Hapo
kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo kisha tukasoma
kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo na leo tunaendelea kuangalia
chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.
Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.
Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.
Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu. Mtu
mwenye vidonda vya tumbo ni mtu mwenye asidi nyingi mwilini kuliko
alkalini, hivyo anatakiwa kupendelea zaidi kula matunda na mboga za
majani. Anahitaji zaidi ukijani mwilini mwake. Pia apendelee kula ugali
wa dona kuliko ugali wa sembe na inashauriwa pia kupunguza kula wali.
Kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni maji. Hakikisha unakunywa kila siku maji glasi 8 hadi 10.
MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI Unalala
chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke,
shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini.
Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk
10
Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5
Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5
Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5
Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki. Hapa
chini nimekuwekea jedwali la jumla la vyakula na vinywaji vyenye asidi
sana, asidi ya kati na alkalini sana, vile vya kuviepuka ni vile vyenye
asidi sana, orodha itaendelea kuboreshwa;
Acid: Viongeza utamu vyote vya kutengenezwa (Artificial Sweeteners)
Nyama
Alkaline:
Neutral:
Acid: Nyama ya ng’ombe, kuku, Samaki, mbuzi, batamzinga, nyama ya nguruwe, Sungura
Mafuta
Alkaline: mafuta ya mbegu za katani
Neutral:
mafuta ya lozi, Canola, mafuta ya nazi, mafuta ya mahindi, Margarine,
mafuta ya zeituni, Safflower, mafuta ya ufuta, mafuta ya Soya, mafuta ya
alizeti
Acid:
Vitafunwa & nafaka
Alkaline: Amaranth, Millet, Quinoa
Neutral:
Acid: Barley, Buckwheat, Oats, mchele, Rye, Spelt, ngano, Pasta (vyakula jamii ya tambi), biskuti
Safu ya kiungo ya Simba ilibadili mchezo
wao wa pasi nyingi hasa baada ya Yanga kuanza mchezo kwa kasi wakitumia
mipira mirefu kutoka kwa Kamusoko kwenda kwa Niyonzima na Ngoma kitu
ambacho kilimfanya Tambwe awe huru zaidi na madhara ya Ngoma yalionekana
kutokana na usumbufu wake akamsababishia kadi Nyekundu mlinzi Banda.
Morali ya wachezaji baada ya Kadi Nyekundu
Wachezaji wa simba walionekana
kutokukubaliana na kadi ya Banda hali ambayo iliwatoa mchezoni kwa muda
akiwemo kiungo Mwinyi Kazimoto ambaye hakucheza kama alivyozoeleka
kwenye Mechi za hivi karbuni na hali hii ilikuja baada ya kiungo Majavi
kulazimika kurudi nyuma kucheza beki na Juuko..Kiungo cha Simba
kilikatika na kutoa nafasi kwa Niyonzima kucheza pamoja na Kamusoko
wakiwalisha vizuri washambuliaji wao.
Kasi na Utulivu wa Donald Ngoma
Ngoma amechangia kwa kiasi kikubwa
ushindi wa jana baada ya kuwa msumbufu na muda wote akikaa eneo la kumi
na Nane ya Simba kitu ambacho kiliwanyima uhuru mabeki wa simba
kuanziana pasi fupi na matokeo yake aliweza kukaa eneo zuri na akatumia
makosa ya Kessy na kuandika bao la kwanza.
Mabadiliko ya Kocha Mayanja
Baada ya mapumziko Kocha wa simba
aliamua kupumzisha Kazimoto ambaye alionekana kuumia na kucheza chini ya
kiwango lakini hakupiga vizuri hesabu zake..kwangu mimi naona alitakiwa
kuingiza beki atakaye cheza na Juuko kisha kumpandisha Majavi kwenye
nafasi ya kiungo wa kati ili kusaidiana na Mkude lakini haikuwa ivyo
aliona amwingize kiungo ambaye bado hakuwa na uzoefu wa pambano kubwa
kama hilo na matokeo yake alipwaya na kumulazimu Ajib kurudi kusaidia
viungo huku mbele wakimwacha Kiiza peke yake.
Kuingia kwa Mwashuya na Simon Msuva
Bao hili liliwatoa simba mchezoni na kuwafanya wacheze nyuma zaidi bila ya kuwa na mashambulizi ya uhakika.
Mechi ilikuwa nzuri kila upande
umejaribu kuonesha nini ambacho wamevuna kwa walimu wao na hatimaye
bahati ikaanguka kwa Yanga na kuibuka na pointi zote sita msimu huu.