Safu ya kiungo ya Simba ilibadili mchezo
wao wa pasi nyingi hasa baada ya Yanga kuanza mchezo kwa kasi wakitumia
mipira mirefu kutoka kwa Kamusoko kwenda kwa Niyonzima na Ngoma kitu
ambacho kilimfanya Tambwe awe huru zaidi na madhara ya Ngoma yalionekana
kutokana na usumbufu wake akamsababishia kadi Nyekundu mlinzi Banda.
Morali ya wachezaji baada ya Kadi Nyekundu
Wachezaji wa simba walionekana
kutokukubaliana na kadi ya Banda hali ambayo iliwatoa mchezoni kwa muda
akiwemo kiungo Mwinyi Kazimoto ambaye hakucheza kama alivyozoeleka
kwenye Mechi za hivi karbuni na hali hii ilikuja baada ya kiungo Majavi
kulazimika kurudi nyuma kucheza beki na Juuko..Kiungo cha Simba
kilikatika na kutoa nafasi kwa Niyonzima kucheza pamoja na Kamusoko
wakiwalisha vizuri washambuliaji wao.
Kasi na Utulivu wa Donald Ngoma
Ngoma amechangia kwa kiasi kikubwa
ushindi wa jana baada ya kuwa msumbufu na muda wote akikaa eneo la kumi
na Nane ya Simba kitu ambacho kiliwanyima uhuru mabeki wa simba
kuanziana pasi fupi na matokeo yake aliweza kukaa eneo zuri na akatumia
makosa ya Kessy na kuandika bao la kwanza.
Mabadiliko ya Kocha Mayanja
Baada ya mapumziko Kocha wa simba
aliamua kupumzisha Kazimoto ambaye alionekana kuumia na kucheza chini ya
kiwango lakini hakupiga vizuri hesabu zake..kwangu mimi naona alitakiwa
kuingiza beki atakaye cheza na Juuko kisha kumpandisha Majavi kwenye
nafasi ya kiungo wa kati ili kusaidiana na Mkude lakini haikuwa ivyo
aliona amwingize kiungo ambaye bado hakuwa na uzoefu wa pambano kubwa
kama hilo na matokeo yake alipwaya na kumulazimu Ajib kurudi kusaidia
viungo huku mbele wakimwacha Kiiza peke yake.
Kuingia kwa Mwashuya na Simon Msuva
Bao hili liliwatoa simba mchezoni na kuwafanya wacheze nyuma zaidi bila ya kuwa na mashambulizi ya uhakika.
Mechi ilikuwa nzuri kila upande
umejaribu kuonesha nini ambacho wamevuna kwa walimu wao na hatimaye
bahati ikaanguka kwa Yanga na kuibuka na pointi zote sita msimu huu.