Sunday

Aliyekua Mshindi Wa Airtel Trace Music Stars 2015 Mayunga Mbioni Kukamilisha Kolabo Yake Na Akon...


Mwimbaji wa Tanzania, Mayunga Nalimi ambaye ni mshindi wa Airtel Trace Music Stars 2015 anatarajia kuondoka nchini Jumatatu (Nov. 16), kuelekea New York, Marekani kwajili ya kurekodi wimbo na mwimbaji mwenye asili ya Senegal, Akon.

Kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Mayunga ametaja mambo matatu anayokwenda kufanya Marekani.

“…naenda kupata hiyo mentorship, kufanya wimbo, na vilevile kushoot video ya wimbo ambao nitaufanya” alisema Mayunga.
Ameongeza kuwa wimbo anaoenda kurekodi utaandikwa na Akon mwenyewe.

“Hiyo ni project ya Akon kwasababu dili ni kwamba atakuwa anakuandikia wimbo yeye…”

Kutokana na ushindi huo, Mayunga alishinda mkataba wa kurekodi muziki na label ya Universal Music Group wenye thamani ya $500,000 ambayo ni takribani shilingi bilioni 1 pamoja na kurekodi wimbo na Akon.

Mwezi July, Mayunga alienda Afrika Kusini kushoot video yake ya kwanza ‘Nice Couple’ ambayo ilitambulishwa exclusive na Trace Urban July 31.

SHARE THIS

0 maoni: