Chama cha soka duniani FIFA kinakataza Serikali kuingilia masuala ya
soka na adhabu kali hutolewa kwa mwanachama yeyote anayekiuka jambo
hilo. Bunge la Uingereza linataka kupiga kura ya kutokuwa na imani na
chama cha soka cha nchini humo FA.
Hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo jambo hili
linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia
nchini Russia ,Endapo bunge litapiga kura wiki ijayo basi itaiweka
Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la
dunia la mwaka 2018.
Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na FA unakuja baada ya baadhi ya
viongozi wa zamani wa FA kudai kwamba chama hicho kinashindwa
kujiendesha.Katika barua ambayo viongozinwa zamani wa FA walimuandikia
mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni bwana Damians Collin inaelezwa
kwamba FA imekwama na imeshindwa kujiendesha.Inasubiriwa kwa hamu kuona
nini kitatokea baada ya kikao cha bunge la Uingereza kutoa maamuzi yao
kuhusu FA.
Kesi hii ya Uingereza haina utofauti na kesi iliyokuwa ikiwakabili
Kuwait katika hatua ya kushiriki kombe la dunia 2018.Serikali ya Kuwait
iliingilia masuala ya soka nchini humo.Wakiwa wamefika raundi ya tatu ya
mechi za kufuzu kombe la dunia FIFA waliamua kuwatoa Kuwait katika
mashindano hayo baada ya serikali yao kukiuka sheria za Fifa.
Uingereza ambao hadi sasa wako katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la
dunia kwani wanaongoza kundi lao la F. Uingereza wamebakiza mechi 6 tu
kufuzu kombe la dunia lakini sheria za FIFA zinaweza kuwazuia kufuzu ama
kuendelea na mechi zao kwa sasa.
0 maoni: