Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) Tawi la
Gezaulole wilayani Hai, Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Hai kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri
wa miaka 7.
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu
anayesikiliza kesi hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi,
Elisha Moleli amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua
kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka
huu nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa
kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za
siri.
Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi
hiyo aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa
yupo rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.
0 maoni: