Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka wasanii nchini
kumuunga mkono katika jitihada zake za kupambana na wezi wa kazi za
wasanii kuliko kuendelea kutoa siri za mapambano yake kwa wahusika
wanaowanyonya wasanii huku akidai wasanii wakubwa wa sekta hiyo hawampi
ushirikiano.
Waziri Nape ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
wadau wa sanaa mbalimbali akieleza baadhi ya wasanii wakubwa wapo
lakini hawatoi ushirikiano wowowte ili hata pale wanapotakiwa kusaidiana
na wizara kupambana na wezi wa kazi za sekta hiyo.
“Nilisema kwenye operesheni hii tuambatane na watu ambao wanafanya
kazi hii, ili waunge mkono kwasababu hii inatakiwa kuwa kama kampeni
tukawaline up wasanii wote wakubwa walikimbia, wewe unajua, wote
walikimbia,” alisisitiza Nape.
“Hata nyinyi wasambazaji wa kazi za ndani sikumuona hata mmoja,
unajua waziri umeenda umefanya operesheni umemaliza mimi nilitegemea
nyinyi mnakaa mnawaita wana habari mnasema tunamuunga mkono waziri na
tutasimama nae kuhakikisha hili jambo linafanikiwa, lakini wote
walikimbia”.
0 maoni: