Serikali imefuta hati ya viwanja 5 vya raia wa Uingereza aliyegushi nyaraka ilhali mkataba wake wa kuishi unaisha mwakani.
Akizungumza na ITV Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi amesema, “Tunafuta hati ya kiwanja kwa kupata hizi title,
sasa leo tunafuta lakini tumemkabidhi Takukuru wamkamate kwasababu
amemiliki kwa taarifa za uongo na tunacho kitambulisho chake
kinachoonyesha kwamba yeye sio raia wa Tanzania ni raia wa Uingereza.”
Ameongeza, “Sasa watu kama hawa tunawajua sasa nawapa tahadhari
wizara yangu kwa kushirikiana na taasisi zingine za serikali kuwa kamata
hawa ambao wamemiliki ardhi yetu ya Tanzania kwa uongo uongo na
udanganyifu. Sisi hati hizi tano tumezifuta kuanzia leo.”
0 maoni: