- *Madaktari, wauguzi, walimu wapeta
- *Wamo pia wa sekta viwanda, kilimo
BAADA ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa,
Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496
kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwanda.
Hata hivyo, licha ya kutaja idadi ya
watumishi wapya wanaotarajiwa kuajiriwa katika mwaka huu wa fedha,
Serikali haijaweka bayana ni lini hasa ajira hizo zitaanza kutolewa
licha ya kuwa imebaki miezi sita mwaka wa bajeti kumalizika.
Akijibu maswali yaliyoulizwa juu ya
lini Serikali itaanza kutoa ajira, baada ya kuzisitisha kwa muda, Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala
Bora), Florence Temba, alisema Serikali inatoa fursa za ajira kama
ilivyoelezwa katika mpango mwaka wa fedha 2016/17.
Katika majibu hayo aliyoyatoa kwa niaba
ya Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, yalibainisha kwamba ajira
hizo zitakuwa kwenye sekta ya elimu, afya, kilimo na mifugo.
KWA HABARI ZAIDI TEMBELA
KWETU FLAVER BLOG KILA WAKATI
KWA HABARI ZAIDI TEMBELA
KWETU FLAVER BLOG KILA WAKATI
ULIITAZAMA HIYO CHINI?:Zari athibitisha yeye na mama mkwe wake bado zinaiva
0 maoni: