Aidha Askofu Mokiwa aliwasili makao makuu ya Dayosisi ya Lweru mjini Muleba mkoani Kagera na alitarajiwa kuungana na maaskofu wengine kumsimika Godfrey Mbelwa kuwa askofu mpya wa dayosisi hiyo.
Lakini taarifa zilizopatikana zimesema Askofu Mokiwa alichukuliwa na polisi na kuhojiwa katika kituo cha Muleba, kutokana na kuhofu kuwa kuwapo kwake kungeweza kusababisha vurugu katika ibada iliyokuwa iongozwe na Dkt. Chimeledya kutokana na mvutano uliopo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Ollomi,amesema kuwa jeshi hilo halikumkamata Askofu Mokiwa na kumhoji, badala yake amesema walichukua hatua haraka baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kuhusu masuala ya usalama. “Ni wajibu wetu kufuatilia, tulimuonya kuhusu suala la kuhudhuria ibada kwa sababu kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani lakini ilikuwa ni hiari yake kutohudhuria, huo utakuwa ni uamuzi wake,” amesema Ollomi.
0 maoni: