Wednesday

Kokoro na Muziki zote zinahit kwa mpango wake – Rich Mavoko

Kuna imani kuwa wimbo wa Darassa, Muziki umezifunika nyimbo nyingi zilizotoka pamoja, ukiwemo Kokoro wa Rich Mavoko aliomshirikisha Diamond.
Hata hivyo Rich amekanusha imani hiyo na kudai kuwa Kokoro na Muziki ni kama Kusini na Kaskazini na kila moja inafanya vizuri.
“Zote hits kwa mpango wake na kila mtu na kila mtu anafanya kitu chake,” Mavoko aliiambia 255 kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM. “Darassa ni mwanamuziki mzuri, uzuri ni rafiki yangu, yaani mimi na yeye ni kama mtu na uncle yake.”
Mavoko amedai kuwa hata kabla wimbo huo haujatoka aliusikia na hata producer aliyeufanya ni mdogo wake, Abbah. Msanii huyo wa WCB pia amemsifia Darassa kwa kuweza kubadilika na kutoa hit single hiyo.
“Kuhusu masuala ya kuitrend Youtube, hizo ni habari za mtaani, unaweza ukagombana na mtu kwa vitu vingine vya kitoto.”
Darassa alimshirikisha Mavoko kwenye wimbo wake uliofanya vizuri pia, Kama Utanipenda.

SHARE THIS

0 maoni: