Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimempongeza Rais Dkt
John Magufuli kwa uchapakazi na utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi
ya chama hicho, lakini pia kwa kuendesha vyema vikao vya kamati kuu ya
chama hicho.
Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa
Dar es Salaam, Juma Simba, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake.
“Rais Magufuli ameendesha vikao kwa muda mfupi, lakini kwa mafanikio
makubwa na sisi kama CCM mkoa tutahakikisha tunashirikiana kwa karibu
zaidi na viongozi wa taifa walioteuliwa hivi karibuni,” alisema Simba.
Aliongeza kuwa pamoja na Rais Magufuli kuendesha vikao hivyo kwa muda
mfupi, lakini ameweza kutoa maamuzi mazito yenye lengo la kukijenga
chama hicho kwa siku moja.
0 maoni: