Tuesday

Alikiba na Vee Money kutupa karata zao kwenye Wana Music Awards Ufaransa Ijumaa hii

Alikiba na Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wa Afrika waliotajwa kuwania tuzo za Wana Music mwaka huu zitakazotolewa nchini Ufaransa, Ijumaa hii (December 30).
Alikiba anawania kipengele cha msanii bora wa kiume wa mwaka akichuana na DJ Arafat, Kiss Daniel, Mr Eazi, Patoranking, Tekno Miles na Wizkid.
Naye Vanessa yupo kwenye kipengele cha msanii bora wa kike wa mwaka akichuana na Akothee, Chidinma, RENISS, Tiwa Savage na Yemi Alade!
Tuzo hizo kwa mwaka huu si za kupigiwa kura kwa mujibu wa waandaji hao.
“Unfortunately there is no vote this year (because we are not so popular for the moment to organize a big vote), it will be our choice. Maybe for the next year,” wameandika kwenye Facebook.

SHARE THIS

0 maoni: