Monday

Ndege ya kijeshi yenye watu 90 yapotea kwenye radar

Ndege ya kijeshi ya Urusi imepotea kwenye radar dakika chache tu baada ya kupaa angani kutoka kwenye mji wa Sochi.
Wizara ya ulinzi imedai kuwa ndege hiyo, Tu-154 ilikuwa na watu 91 wakiwemo wanajeshi, bendi ya jeshi na waandishi wa habari.
Ndege hiyo ilitoweka kwenye radar dakika 20 baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adler. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zimedai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaenda kwenye jimbo la Syria, Latakia.
Msemaji wa wizara ya ulinzi, Igor Konashenkov amedai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaenda kushiriki kwenye mkesha wa mwaka mpya na wanajeshi wa Urusi walioko Syria.
Majeshi ya Urusi, nchi yenye ukaribu na rais wa Syria, Bashar al-Assad yamekuwa yakifanya mashambulio dhidi ya makundi ya kigaidi.

SHARE THIS

0 maoni: