Baada ya msoto na hatimaye
kufanikiwa kimuziki Ambwene Yesaya AY ametangaza rasmi kumpata mtu
atakayesimamia kazi zake (Meneja) ambaye ni Sallam SK meneja mahiri
kabisa wa masuala ya nje wa msanii nyota Diamond Plutnumz.
Meneja huyo wa Diamond
Salaam SK katika mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio amesema
licha ya Ay kuwa na Connections za kutosha pamoja kujisimamia mwenyewe
mda mrefu,ameamua kufanya naye kazi kwasababu ya uwezo mkubwa alionao wa
kushawishi kufanya kazi na watu mbalimbali.
Salaam amesema kuwa na
connection ni jambo moja na kuweza kuzishawishi connections hizo ni
jambo la pili, ingawa haimaanishi AY hawezi lakini amemuamini yeye
kwajinsi alivyoona ushawishi wake.
Pia Salaam ameongeza kuwa katika
menejiment yake hafanyi kazi na mtu ambaye hajitumii katika kazi zake na
kuongeza kuwa msanii lazima awe na ushawishi kwa meneja wake na
kumlazimisha kufanya vitu ambavyo meneja akiona hawezi kuamini kama
vingefanikiwa, akiwa na maana ya wivu wa maendeleo.
0 maoni: