Sunday

IZZO BIZNESS AFUNGUKIA YA JUX, VANESSA NA JACK CLIFF

Rapa mahiri anae uwakilisha vyema mkoa wa  Mbeya Izzobizness amesema kwasasa anamtambua Vanessa kama Shem lake official kwa msanii Jux akiongeza kuwa mahusiano ya Jack Cliff na Jux yalishapita.

Izzo ni mmoja wa marafiki wa karibu wa Jux na wakati anayasema hayo alikuwa pia karibu na Jux kwenye mishe zao.

Izzo alisikika kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio akifafanua kuwa kwa mujibu wa Jux ambaye ni mshkaji wao amewatambulisha rasmi kwa Vanessa na yeye kama rafiki basi anafuata kile mshkaji wake alichosema kuhusu mambo yake binafsi.

Jack cliff ambaye alikuwa mpenzi wa Jux yupo jela nchini China baada ya kukamatwa na dawa za kulevya na sasa Jux anatoka kimapenzi na muimbaji mahiri Vanessa Mdee.

Chanzo mtembezi.com

 

 

 

 


SHARE THIS

0 maoni: