Kuna wakati ‘Wambea’ huwa na
data kamili, lakini hufikisha bila ruhusa, udaku hua unasababisha
mivurugano lakini kuna udaku mwingine huleta furaha na kuzidisha faraja
kwa baadhi ya watu.
Kinacho endelea katika
mitandao mbali mbali ya ‘udaku’ Afrika Mashariki ni eti Diamond ameamua
kupima vinasaba vya damu (DNA) ili kubaini kwamba Latiffah ‘Tiffah’ ni
damu yake ama la.
Kizizi cha taarifa hizi kinasema kipimo hicho kimafanyika Afrika Kusini siku chache kabla staa huyu hajaenda Las Vegas.
Gazeti la Amani kutoka
Tanzania pia limeripoti kufanya mahojiano na Diamond Platnumz. “Kutokana
na maneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda.
Hivyo ili kuondoa figisu
figisu, akamwambia mpenzi wake Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye.
hii ilikiuwa kabla hajaenda Marekani.” alisema Chibu katika mahojiano na
gazeti hilo.
Vipimo vya DNA
vimethibitisha kuwa Tiffah Dangote ni mtoto wa Diamond na sio mtoto wa
billionaire Ivan Semwanga ambaye ni mzazi mwenzie na Zari aliyekaa naye
kwa miaka 10.
Kwa mtazamo wa Tamaduni za
Kitanzania na ‘Ushababi’, nachelea kuliamini hili kwa dhati kwa kuwa
Diamond ni miongoni mwa wasanii thabiti wasioyumbisha na ‘Kijini tope’
cha aina yoyote ile, lakini kama ni kweli ‘kauridhisha mtima wake’.
0 maoni: