Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts

Tuesday

JOKATE AMUANDIKIA ALIKIBA ALIYONAYO MOYONI MWAKE

JOKATE AMUANDIKIA ALIKIBA ALIYONAYO MOYONI MWAKE


Super business woman, Jokate Mwegelo amemuandikia AliKiba ujumbe mzuri ambao amedai umetoka kwenye sakafu ya moyo wake.Mwanamitindo huyo ambaye yupo karibu zaidi na mkali huyo wa wimbo ‘Aje’ amemsifia msanii huyo huku akiichambua show yake aliyoifanya usiku wa kuamkia Jumapili katika tamasha la Fiesta Dar es salaam. Kupitia Instagram, Jokate ameandika:

 Komando Kipensi @officialalikiba kwanza thank you for trusting me and @noelgiotz to style you for Fiesta- tulielewa how important this day is to you and I’m glad we made it . It was fun creating this iconic look, you made it easy though I mean your body is just perfect and the way you carry yourself with so much class and honor you just gave this outfit the life and sophistication it needed. Style yako ya mavazi ni ya kipekee, hugezi mtu unatengeneza yako kama unavyofanya na mziki wako, ni halisi. Sasa mimi napenda kuongea nikiguswa, sio kama AK ila baada ya kuona ulichofanya jana kwenye stage ya fiesta ( umeimba live na band kwenye umati mkubwa vile kwa ustadi mkubwa kabisa mpaka watu wakashtuka maana you were simply perfect ) naomba kusema tu wewe hushindani na yoyote hapa Tanzania, kuanzia ladha yako ya mziki unaotengeneza mpaka sauti yako – tena huko kwenye sauti naomba nisiongee maana sitaki upasuke bichwa lako lol ila kuna kitu cha kipekee kwenye sauti yako, you are “The Voice”. Kila siku unakuwa bora zaidi yaani labda nikufananishe na Beyonce kimziki- usiniue lakini . Ukitaka you can dance, you can sing tena live sauti cleeeear haina mikwaruzo, you can rap, unaeeza igiza uchizi yaani you are just perfect kama mwanamuziki. Kama hujui leo ujue. Nakuombea siku mmoja dunia nzima iweze kufurahia hiki kipaji adhimu kutoka kwako. Unajua kuna tofauti ya kuimba wimbo au kusikiliza wimbo tu kama burudani na kusikiliza kitu kinachokuinua spiritually. Kitu kinagusa roho yako. Nikisikia Aje, Mwana, My Everything, Mali yangu hata kama nina mood mbaya vipi my soul becomes happy yaani naturally. You are a gem na utafika tu. Huu mwendo wako huu huu ndio poa. Wasikuchanganye. Nikiangalia mfano wa Wizkid yeye anafanya mziki wake, focus yake niyeye na fans wake na ndio maana yuko alipo licha ya kushindanishwa na watu kutwa nzima. Blood fans wa AK najua mko nae tumlazimishe huyu kijana afanye tour nchi nzima pekee yake labda . Haya mambo ni makubwa wallahy. All in all I’m very proud of you na your journey of growth and WTH man start giving me credit on the lyrics I help you with . Hongera @cloudsfmtz kwa show nzuri na kwa wasanii wote #Kajiandae #KingKiba #Kidoti

Thursday

YAKUZINGATIA WAKATI WA KUMUOMBA MSAMAHA MPENZI WAKO

YAKUZINGATIA WAKATI WA KUMUOMBA MSAMAHA MPENZI WAKO


Kukosea katika maisha ya binadamu ni kawaida pia ni sehemu ya maisha, inaaminika kwamba kukosea ni kujifunza, maana kosa utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika mahusiano ya kimapenzi

Hakuna cha ajabu ni kawaida kabisa lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna gani tunajifunza kupitia makosa, ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti hizo, maana unaweza kuwa hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe, lakini wimbo huo ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku, Mtembezi Mahaba inakuletea njia pekee za kuomba msamaha kama ifuatavyo

KOSA LINA UKUBWA GANI?
Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwa sababu hujamwambia chochote, naye hana raha na wewe, hivyo hatokuwa na amani ya moyo.

Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo, kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri  wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani?

ONESHA UNAVYOJUTA
Hii ni kwa ajili yako wewe mwenyewe, rafiki zangu, kutakuwa hakuna maana yoyote kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo, kama msamaha wako haujatoka moyoni.

Ukiwa peke yako, jiaminishe kwamba umekosea na kwa hakika unahitaji kusamehewa, jutia ndani ya moyo wako, kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi kwamba hutarudia tena,hili ni zoezi la kisaikolojia, ambalo litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi wako kwa ajili ya kuomba msamaha.

KUWA MKWELI
Omba kukutana naye yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini hapa jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wa karibu  na yeye. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.

Mwambie jinsi unavyoteseka na jinsi msivyo katika maelewano mazuri, kauli yako ya ukweli, hisia zako wakati wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka katika mazingira mazuri ya kuweka mambo sawa.

MHAKIKISHIE HUTORUDIA KOSA
Bila shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini, uwezekano wa kusamehewa ni mkubwa sana na haya ndiyo matarajio yangu, naamini hata wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie mpenzi wako kuwa hutorudia tena.

Mwambie kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya tena asiwe mnyonge, hakuna uchawi ni maneno tu!

 FANYA KITU MAALUM
Hapa unatakiwa kufanya kitu maalumu kwa ajili ya mpenzi, ukionesha kwamba umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu utakachokifanya hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema awali.

Mathalani unaweza kutoka naye na kwenda kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa mahaba mazito kama shukrani kwake. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kulingana na uwezo wako kifedha. Fanya vyovyote ili kosa lile lisahaulike moja kwa moja.

Tuesday

NJIA 5 ZA KUMFANYA MWANAMKE AKUFUKUZIE BAADA YA KUMUONESHA HISIA

NJIA 5 ZA KUMFANYA MWANAMKE AKUFUKUZIE BAADA YA KUMUONESHA HISIA


Najua huwa tunatumia muda  mwingi sana vijiweni tukiongelea, sehemu gani nzuri ya kukutana na wanawake, jinsi ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini cha kuongea na kufanya ili akuelewe na mrembo awe wako, Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea huwa ni kama theluji kwenye mlima Kilimanjaro, ila volkano yenyewe huwa ni jinsi ya kuwafanya wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na hizi hapa ni njia tano za kuwa wapekee na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.

Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia hizi hakikisha hauzichukulii juu juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye akili yako, maana unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu wanawake.

Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.

Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa Kutongoza toka moyoni bila hata kufikiria utaongea nini au kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza kujitambulisha, “Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba”, mwenyewe anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.

Namba 2. Muonyeshe changamoto.

Mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo), mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye mapenzi yanamuendesha.

Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.

Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna uhakika mkubwa ataendelea kukufikiria kuwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi, na unajua wanawake wanahisia gani na wanaume wa aina hii. Kwahiyo ukianza na maswali ya kuonyesha tabia ya kifala, patishia huyo mwanamke ataanza kukufikiria kuwa utakuwa na tabia hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huo ndo utakuwa mwisho wako.

Namba 4. Usimfuatilie sana.

Usipoonana na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako, iwapo ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo ukiwa unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubiri na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia, utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja.

Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani. Wanawake wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo hazihitajiki

Chanzo mtembezi.com