Kukosea katika maisha ya binadamu ni
kawaida pia ni sehemu ya maisha, inaaminika kwamba kukosea ni kujifunza,
maana kosa utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika
mahusiano ya kimapenzi
Hakuna cha ajabu ni kawaida kabisa
lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna gani tunajifunza kupitia
makosa, ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti hizo, maana unaweza kuwa
hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe, lakini wimbo huo
ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku, Mtembezi Mahaba inakuletea njia
pekee za kuomba msamaha kama ifuatavyo
KOSA LINA UKUBWA GANI?
Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba
unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwa sababu hujamwambia chochote,
naye hana raha na wewe, hivyo hatokuwa na amani ya moyo.
Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari
ukubwa wa tatizo, kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri wa
jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango
gani?
ONESHA UNAVYOJUTA
Hii ni kwa ajili yako wewe mwenyewe, rafiki zangu, kutakuwa hakuna maana
yoyote kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo,
kama msamaha wako haujatoka moyoni.
Ukiwa peke yako, jiaminishe kwamba
umekosea na kwa hakika unahitaji kusamehewa, jutia ndani ya moyo wako,
kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi kwamba hutarudia tena,hili ni zoezi la
kisaikolojia, ambalo litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi
wako kwa ajili ya kuomba msamaha.
KUWA MKWELI
Omba kukutana naye yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini
hapa jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wa karibu na
yeye. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.
Mwambie jinsi unavyoteseka na jinsi
msivyo katika maelewano mazuri, kauli yako ya ukweli, hisia zako wakati
wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka katika mazingira mazuri ya kuweka
mambo sawa.
MHAKIKISHIE HUTORUDIA KOSA
Bila shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini,
uwezekano wa kusamehewa ni mkubwa sana na haya ndiyo matarajio yangu,
naamini hata wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie
mpenzi wako kuwa hutorudia tena.
Mwambie kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya tena asiwe mnyonge, hakuna uchawi ni maneno tu!
FANYA KITU MAALUM
Hapa unatakiwa kufanya kitu maalumu kwa ajili ya mpenzi, ukionesha
kwamba umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu
utakachokifanya hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema
awali.
Mathalani unaweza kutoka naye na kwenda
kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa mahaba mazito kama shukrani
kwake. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kulingana na uwezo wako
kifedha. Fanya vyovyote ili kosa lile lisahaulike moja kwa moja.
0 maoni: