Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Yusuph Masaun
amepiga marufuku ununuzi wa sare za jeshi la zima moto na uhamiaji kwa
taasisi binafsi na badala yake ameagiza sare hizo zizalishwe katika
viwanda vya jeshi la magereza nchini.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo baada ya kutembelea kiwanda cha jeshi
la magereza kilichopo Ukonga kinachoendeshwa kwa nguvu kazi ya wafungwa
ikiwa ni ufuatiliaji, utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania la kulitaka jeshi hilo liwasimamie wafungwa katika
uzalishaji wa sare.
“Kuanzia leo uhamiaji zima moto wote washone nguo, kama ambapo
magereza wanashona katika kile kiwanda, kwamba dhamira ya mheshimiwa
rais ya kutoa maelekezo ambayo yamefuatilia utendaji kazi wake
nimeridhika, kwamba ni marufuku kama alivyosema mheshimiwa rais kwa
askari Magereza na askari wote wa vyombo vya usalama nchini kununua
uniform kwa raia, jeshi la magereza linatengeza furniture zenye ubora
wa hali ya juu,” alisema Mhandisi Masauni.
SHARE THIS
0 maoni: