Wednesday

Nape Nnauye amemteuwa Mkurugenzi mpya wa Idara ya Maendeleo ya Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, Jumatano hii amemteuwa Yusuph Singo Omari kuwa Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya michezo akichukuwa nafasi ya Leonard Thadeo aliyehamishiwa katika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Awali Singo alikuwa ni mkufunzi mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Ardhi katika masuala ya michezo. Uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 katika kifungu 6(1)(b) pamoja na kifungu namba 8 ya sheria hiyo.
Soma taarifa hiyo hapa chini.

SHARE THIS

0 maoni: