Waziri Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema
amesikia kilio cha wasanii kuhusu kuwabana katika kazi zao hususan
kwenye video za muziki na kuahidi kufumba jicho moja ili kuwapa uhuru
kiasi.
Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye tuzo za EATV zilizotolewa
kwa mara ya kwanza Jumamosi hii kwenye ukumbi wa Mlimani City.
“Tutaachia kidogo hatutabana sana, “alisema Nape. “Na mimi nimepita
mtaani naambiwa ‘Nape mmebana sana.’ Wakati mwingine tunataka kufanya
mambo tunaambiwa tumepitiliza. Wakati mwingine tutafumba jicho moja watu
wapitilize kidogo ili mambo yaende sawa sawa,” alisisitiza waziri huyo
aliyekuwa mgeni rasmi kwenye tuzo hizo.
Kwa muda mrefu Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA lililo chini ya
wizara yake, limekuwa likilaumiwa kwa kutoa adhabu kali kwa wasanii kwa
kile inachosema ni kuvunja maadili.
0 maoni: