Akiongea na gazeti la Habari Leo wiki hii, Mwana FA alisema bifu la wasanii hao linachangamsha tasnia ya muziki na kusisitiza muhimu ni kudhibiti wasizuriane.
“Unajua hakuna kitu kisichokuwa na ushindani, mfano wewe upo Daily News lazima mtakuwa na washindani wenu, mnachotakiwa kufanya ninyi waandishi ni kujizuia msizuriane,” alisema FA.
“Inachangamsha muziki unapata wa kuwazungumzia, kukiwa na ushindani wa hapa na pale sifikiri kama ni kitu unachoweza kukizuia, game ikiwa rafiki sana nayo inakuwa haiwezi kuburudisha, haiwezekani mashabiki wawe wote wa wanamuziki wote hakuna kitu kama hicho,” aliongeza.
Pia rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Dume Suruali’ amedai kwa sasa bado ana mambo mengi ya kufanya katika kuendeleza muziki wake lakini pia kuendeleza familia yake pamoja na masuala ya biashara.
0 maoni: