Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Edward Lowassa amevunja ukimya kuhusu mgogoro wa uhalali wa Uenyekiti wa
Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya
siasa unaoendelea ndani ya chama cha wananchi CUF.
Lowassa ambaye alitajwa na Profesa Lipumba kuwa chanzo cha yeye
kujiuzulu kabla ya kurejea tena miezi tisa baadaye kutengua uamuzi wake,
amesema kuwa kushindwa kwa chama hicho ni kushindwa kwao na vyama vyote
vinavyounda UKAWA.
Mjumbe huyo alitumia ukurasa wake wa Facebook kueleza jinsi ambavyo
Ukawa inalibeba tatizo la mgogoro unaendelea ndani ya chama cha CUF.
“CUF ni wenzetu katika Ukawa. Shida zao ni shida zetu, vita vyao ni vita
vyetu, kushindwa kwao ni kushindwa kwetu, ushindi wao ni ushindi wetu,”
aliandika Lowassa.
Profesa Ibrahim Lipumba amekuwa akieleza kuwa hayuko tayari kuona Chadema au Lowassa wanakinunua chama hicho.
0 maoni: