Unataka kufanya collabo na Ben Pol? Muwahi sasa kabla ya Disemba 31, sababu mwaka 2017, mambo yanakwenda kubadilika.
Ben Pol amesema kuanzia mwakani atakuwa akitoa dola 5,000 kwa kila kolabo ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Kitanzania.
“Kuelekea 2017 bei yangu ya Collabo itakuwa $5000. So kama una
project na mimi tuwasiliane before 31st Dec 2016,” aliandika Ben kwenye
Twitter.
“Ni kweli, ila kama wimbo ni mkali tunaweza kukaa mezani na huyo mtu
akanipa sehemu ya umiliki wa hiyo kazi,” Ben ameiambia Bongo5 baada ya
kumuuliza kama amedhamiria kweli.
“Kwanza nataka kupunguza idadi ya colabo ili nifanye chache za walio
serious na wanaoweza kupush hizo project. Mfano mtu hawezi kukulipa dola
elfu 5 halafu akaiweka ngoma kwenye album, au akaiweka ndani tu,”
amesisitiza.
“Pia itasaidia kwangu kufikiria zaidi kwenye hiyo kazi, hakuna mtu
atakulipa dola 5 halafu akatarajia disappointment, so ita-benefit kwa
pande zote.”
0 maoni: