Mwanasiasa wa upizani Samy Badibanga atangazwa kuwa waziri mkuu DRC
Mwanasiasa wa upizani Samy Badibanga, ametagazwa kuwa waziri mkuu nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo ,kufuatia makubaliano yaliyokumbwa na utata kati ya serikali na wapizani kwa kuahirisha uchanguzi wa urais hadi April 2018.
Uchanguzi mkuu ulistahili kufanyika mwezi huu ambapo wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa mwisho.
Makubaliano hayo yameongeza hatamu ya uongozi kwa Joseph Kabila.
Ni siku tatu tangu waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, kujiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu pamoja na bwana Ponyo.
0 maoni: